KWA
HALI HII, MUHIMU SANA KWA UKAWA KUANZISHA KIKOSI MAALUM CHA AMANI, ULINZI NA
USALAMA WA UKAWA......
Wadau wa fikra pevu na wachambuzi wa
mwenendo wa kisiasa TZ, hali hii ya uonevu na unyanyasaji wa kisiasa inatisha,
kinyume na Demokrasia, Amani na Utilivu ambavyo ndio msingi wa ustawi wa Jamii
yoyote.
Kwa yaliyomkumba Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA
Prof Ibrahim H. Lipumba, ambaye ni MKiti wa CUF, chama ambacho kinatawala Z'Bar
kupitia Katibu wake aliye makamo wa Rais, ni ufidhuli, uvurugaji na utokomezaji
wa HAKI, DEMOKRASIA NA
KUVURUGA AMAANI.
Kuna haja ya UKAWA kufanya KIKAO cha
Dharura na kuafiki mbinu bora, sahihi na za msigi kuanzisha kikosi cha AMANI,
Ulinzi na Usalama cha UKAWA, ambacho ikiafikiwa kitambukike kama 'UKAWA WHITE
BRIGADE-15' au kwa kifupi UWB-15); Kitakuwa Kikosi maalum CHA AMANI NA UTULIVU
wa TAIFA JIPYA, na hasa Viongozi wake.
Tafsiri: Dhana 'WHITE' = Amani na Utulivu
[Kusimamia HAKI, AMANI NA UTULIVU hadi inapotokea hatari NDIO wachukue action
kali na stahiki kulinda], na namba -15,= yaani Mwaka 2015, mwaka ambao UKAWA
inaelekea kulikomboa Taifa na kuzaa Taifa jipa la Tanganyika, kutoka ktk mikono
ya utawala wa mabeberu na ma-nazi meusi CCM. Wayafanyao watawala hawa
yanajidhihirisha wazi kuvunjika kwa utawala. Huwa hatua ya kwanza za tawala
zinazoanguka ni kueneza woga kwa wanaotaka kujenga fikra huru, kutisha watu na
kuzuia hisia za fikra mpya, kuvuruga kujiamini na kuchochea mgawanyiko. Ndio
tunayoyaona sasa, na tutayaonana matukio mengi zaidi kwa jinsi tunavyosogea
uKOMBOZI na kuchagua utawala mpya Oktoba 2015! Tusichelewe kuchukua maamuzi ya
muhimu.
Naomba kuwasilisha!

No comments:
Post a Comment