Wananchi waapisha viongozi - Tabata
Segerea
Na Stephen kitomary
VIONGOZI wa serikali ya mtaa wa Migombani,
kata ya Segerea, wilaya ya Ilala, wameapishwa na wananchi. MwanaHALISIonline linaandika.
Kiapo hicho
kimefanyika leo, baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kushidwa kutimiza
wajibu wake kwa muda uliopagwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi wa
serikali za mitaa, vijiji na vitongoji za mwaka 2014.
Wakizungumza
na MwanaHALISIonline, wakazi wa mtaa huo wamesema, kutoapishwa kwa viongozi wa
waliowachagua kumeathiri masuala ya maendeleo katika eneo hilo, hali
iliyopelekea kuchukua uamuzi wa kumuita wakili anayetambulika kisheria
kuwaapisha viongozi wapya.
“Wananchi
wamechoka. Wameamua kubadilisha uongozi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukiweka
Chama cha Demokrasi na maendeleo cha Chadema Madarakani ….
“Lakini
tayari zimepita siku 30 bila viongozi kuapishwa. Mkurugenzi wa Halmashauri,
Issaya Mungurumi, haijatoa sababu ya msingi ya kushidwa kuwaapisha viongozi.
Tumeamua kuchukua jukumu hilo sisi wenyewe kwa sababu ndiyo tunaopata shida,”
amesema Obedi John, mkazi wa mtaa huo.
Akizungumza
na MwanaHALISIonline baada ya kuapishwa, Mwenyekiti wa Mtaa huo Japhet Albert
Kembo amesema “wananchi wamechoka kukaa bila huduma za serikali ya mtaa, leo
saa 2:30 asubuhi wamekuja nyumbani kwangu na kunitaka niende ofisi ya serikali ya mtaa nikaapishwe”
Kiapo hicho
kimefanyika nje ya ofsi ya serikali ya mtaa chini ya Wakili wa kujitegemea Iddi
Msawangu, huku ofisi zikiwa zimefugwa na Afisa mtendaji wa mtaa, Suzan Zephania
akitoweka kusiko julikana dakika 20 kabla ya tukio hilo kuanza.
Msawangu
amesema “Leo nimewaapisha viongopzi wa serikali ya mtaa akiwemo mwenyekiti,
wajumbe watatu wa kamati ya mtaa waliohudhuria, huku wajumbe wengine wakiomba
udhuru.”
Aidha,
Msawangu amesema amefanya kazi hiyo baada ya kuobwa na wananchi ikiwa ni sehemu
ya kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Issaya Mungurumi,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, alipotafutwa kwa njia ya simu
na MwanaHALISIonline, kuzungumzia tukio hilo amejibu kwa kifupi “ Sina taarifa
kuhusu viongozi kuapishwa na wananchi. Zipo sababu za msingi za kucheleweshwa
kwa zoezi hilo kwa mitaa mitatu. Ukinitafuta ofsini kwangu, nitakueleza kwa
undani. Tunatarajia kuwaapisha viongozi ndani ya wiki hii”
Mungurumi
alipoulizwa ni sababu zipi zilizochelewesha uapishwaji amesema “ Kwa sasa
siwezi kuongea. Nipo Kwenye kikao nitafute wakati mwingine.”
Samweli
Binagi, aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa huo kwa tiketi ya CCM amesema “kama
wananchi wameamua kuchukua hatua hiyo ambayo haina tatizo la kisheria mimi sina
tatizo na umauzi waliouchukuwa wa kuwaapisha viongozi waliowachagua.”
Mtaa wa
Migombani, anakoishi Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masuburi ulifanya
uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa 14 Desema, 2014 huku Mgombea wa
Chadema Japhet Albert Kembo akishinda kwa kura 547 kati ya kura 1057 zilizopigwa
huku idadi ya waliojiandikisha ikiwa ni 1565.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na mgombea wa CCM, Uyeka Lumbyambya alipata kura 273 huku
nafasi ya tatu ikichukuliwa na mgombea wa NCCR Mageuzi Elick Mchata aliyepata
kura 205.
Aidha,
uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya mtaa ulifanyika 21 Desemba, 2014 na Chadema
kushinda viti vyote.
mwisho

No comments:
Post a Comment