Wednesday, 28 January 2015

KWA HALI HII, MUHIMU SANA KWA UKAWA KUANZISHA KIKOSI MAALUM CHA AMANI, ULINZI NA USALAMA WA UKAWA......


    Wadau wa fikra pevu na wachambuzi wa mwenendo wa kisiasa TZ, hali hii ya uonevu na unyanyasaji wa kisiasa inatisha, kinyume na Demokrasia, Amani na Utilivu ambavyo ndio msingi wa ustawi wa Jamii yoyote.

    Kwa yaliyomkumba Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Prof Ibrahim H. Lipumba, ambaye ni MKiti wa CUF, chama ambacho kinatawala Z'Bar kupitia Katibu wake aliye makamo wa Rais, ni ufidhuli, uvurugaji na utokomezaji wa HAKI, DEMOKRASIA NA KUVURUGA AMAANI.

    Kuna haja ya UKAWA kufanya KIKAO cha Dharura na kuafiki mbinu bora, sahihi na za msigi kuanzisha kikosi cha AMANI, Ulinzi na Usalama cha UKAWA, ambacho ikiafikiwa kitambukike kama 'UKAWA WHITE BRIGADE-15' au kwa kifupi UWB-15); Kitakuwa Kikosi maalum CHA AMANI NA UTULIVU wa TAIFA JIPYA, na hasa Viongozi wake.

    Tafsiri: Dhana 'WHITE' = Amani na Utulivu [Kusimamia HAKI, AMANI NA UTULIVU hadi inapotokea hatari NDIO wachukue action kali na stahiki kulinda], na namba -15,= yaani Mwaka 2015, mwaka ambao UKAWA inaelekea kulikomboa Taifa na kuzaa Taifa jipa la Tanganyika, kutoka ktk mikono ya utawala wa mabeberu na ma-nazi meusi CCM. Wayafanyao watawala hawa yanajidhihirisha wazi kuvunjika kwa utawala. Huwa hatua ya kwanza za tawala zinazoanguka ni kueneza woga kwa wanaotaka kujenga fikra huru, kutisha watu na kuzuia hisia za fikra mpya, kuvuruga kujiamini na kuchochea mgawanyiko. Ndio tunayoyaona sasa, na tutayaonana matukio mengi zaidi kwa jinsi tunavyosogea uKOMBOZI na kuchagua utawala mpya Oktoba 2015! Tusichelewe kuchukua maamuzi ya muhimu.

    Naomba kuwasilisha!

Saturday, 24 January 2015

RAIS KIKWETE AENDELEA KUDHIHIRISHA UMMA WA WATANZANIA WELEDI WAKE MDOGO WA MFUMO MBOVU WA KUSHINDWA KUWAWAJIBISHA MAWAZIRI WANAO HARIBU KTK WIZARA ZAO NA KUFANYA MAZINGA UMBWE YA KUWABADILISHA


UNGANA NAMI   (  KITOMARY)

 
 
Saa chache tu baada ya Profesa Sospeter Muhongo waziri wa nishati na madini wa Tanzania kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na sakata la Escrow,rais Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Jioni hii Ikulu Amefanya mkutano wa ghafla na waandishi wa habari,uliofanyika ikulu jijini Dar es salaam

Hawa ndiyo Mawaziri 8 Mizigo walioteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo
 
1.George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
2.Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
3.Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
4.Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5.Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
6.Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
7.Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge
 
8.Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji

Manaibu Waziri  5 walioteuliwa
1.Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
2.Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
3.Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4.Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5.Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini


Nafasi ya Profesa Sospeter Muhongo aliyekuwa waziri wa nishati na madini imechukuliwa na George Simbachawene huku nafasi ya Profesa Anna Tibaijuka aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikichukuliwa na William Lukuvi.


 Charles Mwijage sasa ni naibu Waziri wa Nishati na Madini akichukua nafasi ya Steven Masele ambaye sasa ni
naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano  


Rais Kikwete amewaapisha  mawaziri hao na manaibu waziri wapya hao ikulu jijini Dar es salaam kuanzia saa 18:10hrs amemaliza saa 18:40hrs kisha zoezi la kupiga picha za pamoja na wateule hao likaendelea..... 
KAZI KWENU WATANZANIA KUWENI MAKINI KWA KUWAPIMA NA KUWAKATAA BAADA YA KUBAINI UWEZO WAO AMBAO NINA UWAKIKA WOTE NI MIZIGO TU AMBAYO IMEBADILISHWA MAKONTENA TU!



                                                   POSTED BY KITOMARY -0719 019 262       
Wananchi waapisha viongozi - Tabata Segerea
Na Stephen kitomary
VIONGOZI wa serikali ya mtaa wa Migombani, kata ya Segerea, wilaya ya Ilala, wameapishwa na wananchi. MwanaHALISIonline linaandika.
Kiapo hicho kimefanyika leo, baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kushidwa kutimiza wajibu wake kwa muda uliopagwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji za mwaka 2014.
Wakizungumza na MwanaHALISIonline, wakazi wa mtaa huo wamesema, kutoapishwa kwa viongozi wa waliowachagua kumeathiri masuala ya maendeleo katika eneo hilo, hali iliyopelekea kuchukua uamuzi wa kumuita wakili anayetambulika kisheria kuwaapisha viongozi wapya.
“Wananchi wamechoka. Wameamua kubadilisha uongozi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukiweka Chama cha Demokrasi na maendeleo cha Chadema Madarakani ….
“Lakini tayari zimepita siku 30 bila viongozi kuapishwa. Mkurugenzi wa Halmashauri, Issaya Mungurumi, haijatoa sababu ya msingi ya kushidwa kuwaapisha viongozi. Tumeamua kuchukua jukumu hilo sisi wenyewe kwa sababu ndiyo tunaopata shida,” amesema Obedi John, mkazi wa mtaa huo.
Akizungumza na MwanaHALISIonline baada ya kuapishwa, Mwenyekiti wa Mtaa huo Japhet Albert Kembo amesema “wananchi wamechoka kukaa bila huduma za serikali ya mtaa, leo saa 2:30 asubuhi wamekuja nyumbani kwangu na kunitaka  niende ofisi ya serikali ya mtaa nikaapishwe”
Kiapo hicho kimefanyika nje ya ofsi ya serikali ya mtaa chini ya Wakili wa kujitegemea Iddi Msawangu, huku ofisi zikiwa zimefugwa na Afisa mtendaji wa mtaa, Suzan Zephania akitoweka kusiko julikana dakika 20 kabla ya tukio hilo kuanza.
Msawangu amesema “Leo nimewaapisha viongopzi wa serikali ya mtaa akiwemo mwenyekiti, wajumbe watatu wa kamati ya mtaa waliohudhuria, huku wajumbe wengine wakiomba udhuru.”
Aidha, Msawangu amesema amefanya kazi hiyo baada ya kuobwa na wananchi ikiwa ni sehemu ya kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Issaya Mungurumi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, alipotafutwa kwa njia ya simu na MwanaHALISIonline, kuzungumzia tukio hilo amejibu kwa kifupi “ Sina taarifa kuhusu viongozi kuapishwa na wananchi. Zipo sababu za msingi za kucheleweshwa kwa zoezi hilo kwa mitaa mitatu. Ukinitafuta ofsini kwangu, nitakueleza kwa undani. Tunatarajia kuwaapisha viongozi ndani ya wiki hii”
Mungurumi alipoulizwa ni sababu zipi zilizochelewesha uapishwaji amesema “ Kwa sasa siwezi kuongea. Nipo Kwenye kikao nitafute wakati mwingine.”
Samweli Binagi, aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa huo kwa tiketi ya CCM amesema “kama wananchi wameamua kuchukua hatua hiyo ambayo haina tatizo la kisheria mimi sina tatizo na umauzi waliouchukuwa wa kuwaapisha viongozi waliowachagua.”

Mtaa wa Migombani, anakoishi Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masuburi ulifanya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa 14 Desema, 2014 huku Mgombea wa Chadema Japhet Albert Kembo akishinda kwa kura 547 kati ya kura 1057 zilizopigwa huku idadi ya waliojiandikisha ikiwa ni 1565.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na mgombea wa CCM, Uyeka Lumbyambya alipata kura 273 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mgombea wa NCCR Mageuzi Elick Mchata aliyepata kura 205.
Aidha, uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya mtaa ulifanyika 21 Desemba, 2014 na Chadema kushinda viti vyote.
mwisho











Tuesday, 13 January 2015

Monday, January 12, 2015

SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR JANA 









MAKAMU WA RAIS GHARIB BILALI  AKISALIMIANA NA JAJI MKUU WA ZANZIBAR KUSHOTO NI RAIS WA AWAMU YA TATU   BENJAMIN .W. MKAPA AMBAYE PIA NI
MSANII NA MTUNZI WA MASHAIRI YA KISWAHILI AMBAYE PIA NI KADA WA CCM MRISHO MPOTO AKISHUHUDIA MATUKIO YA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR..PICHA NA KITOMARY
WASANII WA NYIMBO ZA MWAMBAO WA PWANI WALIO HUDHURIA KWENYE HAFLA HIYO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

MPIGA PICHA MKUU WA RAIS WA ZANZIBAR AKIWA KAZINI..
BAADHI YA VIONGOZI WA SMZ WAKISHUHUDIA MATUKIO MBALIMBALI YA SHEREHE ZA KUMBUKUMBU ZA MIAKA 51 YA MAPINDUZI MATAKATIFU YA KUMUONDOA SULTANI..