MATUKIO-KITOMARY
Matukio haya na yale sambamba na habari/picha za ziada za Globu ya Jamii
Wednesday, December 3, 2014
UWEZO WA VYUO VIKUU KUCHUKUA WANAFUNZI WA SAYANSI BADO CHANGAMOTO KWA TANZANIA KUTIMIZA MALENGO YA EFA
Waziri
wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa
akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za
utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA
uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango
huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea
kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.(Picha na
Zainul Mzige wa MOblog).
Tanzania
imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini
mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa
wote (EFA).Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa
wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini
Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani
imeweza kukaribia kufikia malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala
la wastani wa waalimu kwa wanafunzi.
Amesema
kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi
47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu
mmoja kwa wanafunzi 27. Mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya mpango
huo ni kuboresha wastani wa wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania
Bara wastani umetoka kuwa wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi
65 huku Zanzibar wastani ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza wakati wa
mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto
zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu
kwa Wote –EFA ulioshirikisha wadau wote wa sekta ya elimu uliofanyika
jijini Dar Es Salaam. Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuiandaa
Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mashauriano ya kiserikali
baina nchi mbalimbali na kuhakikisha wadau wakuu wa elimu kitaifa
wanapata taarifa juu ya mapendekezo ya agenda zitakazoanza mwaka 2015.
Awali
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema
ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo
Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati
ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.
Bi.
Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na
Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo
kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na
kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha ,
wadau, usimamizi na uwajibikaji.
BENKI YA CRDB YASAINI MKATABA WA HALI BORA ZA WAFANYAKAZI WAKE
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa
uwekaji saini wa Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi na Chama cha
Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) uliofanyika jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga na
Katibu wa Benki, John Rugambo.
Baadhi ya maofisa wa CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO),
Shikunzi John akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga, Katibu wa Benki, John Rugambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga, Katibu wa Benki, John Rugambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati)
akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka wa benki hiyo na Katibu Mkuu
Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akisaini
mkataba wa hali bora za wafanyaka na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha
Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John (wa pili kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei
(wa pili kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya
Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi wa benki hiyo na TUICO jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei
(kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya
Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi kati ya Chama hicho na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB na
imetiliana saini mkataba na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda,
Huduma na Biashara (TUICO) wa kuboresha hali bora za wafanyakazi wa benki hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema
mafanikio yoyote ya kibiashara hayapatikani kama wafanyakazi ambao ndio
wazalishaji hwatakuwa na mazingira yenye maslahi bora na motisha mbalimbali.
Dk. Kimei
alisema nia ya CRDB ni kuboresha mahusiano kati ya mwajiri na wafanyakazi,
kuboresha mazingiraya utendaji kazi ili kuchochea ufanisi, kurasimisha
mahusiano kati ya benki na wafanyakazi kwa kuweka miongozo itakayosaidia
kupunguza mifarakano kati ya CRDB na wafanyakazi.
“Mkataba huu ni
wa miaka mitatu, utasaidia kuajiri na uthibitishwaji wa wafanyakazi kazini, kushughulikia
migogoro ya kikazi, uhamisho wa viongozi wa chama cha wafanyakazi sehemu ya
kazi,utaratibu wa likizo ya uzazi, likizo ya ugonjwa, ulipwaji gharama ya
usafirishaji mizigo kwa wafanyakazi wanaohamishwa, mazishi ya wazazi wa
wafanyakazi, bima na utoaji tuzo,”alisema
Aidha alisema
WAJASIRIAMALI WAELEZEA WALIVYOWEZESHWA NA PROMOSHENI YA SAFARI LAGER WEZESHWA YA TBL
Jacquline
Shija Mazemle, aliyewezeshwa na TBL na kufanikiwa kuanzisha mghahawa
maarufu wa FACEBOOK, ulioko karibu na Chuo Kikuu cha Kampala, Gongo la
Mboto, Dar es Salaam.
Akiandaa chakula na wenzake Ramadhan Seleman kushoto na Hans Shija
Akiwahudumia na wateja wa Facebook
Dorren akionyesha mashine ya zamani
Dorren kulia na msaidizi wake Ali Chares
Dorren Assei akionesha moja ya majiko ya kuokea mikate
Hapa ndio Facebook
Jacquline Shija akielezea kuhusu mafanikio yake baada ya kuwezeshwa na Safari Lager Wezeshwa
Akiandaa chakula na wenzake Ramadhan Seleman kushoto na Hans Shija
Akiwahudumia na wateja wa Facebook
Dorren Asey aliyewezeshwa na TBL kutengeneza mikate, keki na maandazi kupitia kampuni yake ya Dee Bakery,Doreen akiandaa mikate
Doreen akiandaa mikateDorren akionyesha mashine ya zamani
Dorren kulia na msaidizi wake Ali Chares
Dorren Assei akionesha moja ya majiko ya kuokea mikate
Hapa ndio Facebook
Jacquline Shija akielezea kuhusu mafanikio yake baada ya kuwezeshwa na Safari Lager Wezeshwa
Tuesday, December 2, 2014
UZUSHI WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI KUVUNA WANACHAMA 167 KUTOKA UKAWA SIYO KWELI ILIKUWA MICHEZO YA KUIGIZA NA WALIO NUNULIWA KUFANIKISHA HAYO WAMEFUNGUKA! NA KUDAI WALIRUBUNIWA KUFANYA HIVYO NA KUTAPELIWA KIASI CHA PESA WALICHO AHIDIWA. CCM CHAFUUU!
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Kulia akimsikiliza Aliyekuwa
Mwenyekiti Baraza la Vijana la Chama cha wananchi CUF Wilaya ya Morogoro
Ndugu Mariam Iswili aliyeamua Kurudisha Kadi ya Cuf na Kujiunga na
Chama cha Mainduzi.Katika Tukio Hilo jumla ya wanacha 167 Kutoka Vyama
vya CUF CHADEMA na NCCR MAGEUZI Walirudisha kadi zao na kusema vyama
hivyo havina sera Mya zaidi ya Majungu na Maneno Mengi yasiyo na Tija
kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Kiwa na Kadi ya Cuf aliyoiokea.
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akionyesha kazi alizokabidhiwa
kuto kwa wanachama waliohama kutoka vyama vya CHADEMA na CUF na
Kuhamia CCM
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Za vyama vya chadema CUF na
Nccr Mageuzi alizookea Kutoka kwa wanachama wa Vyama Hivyo na Kuamua
Kujiunga na chama cha Mapinduzi .
Waliokuwa wanachama wa Ukawa wakila kiao mara baada ya Kukabidhiwa kadi za CCM
Wanafunzi Tisa (9) -Wahitimu mafunzo ya uuguzi na ukunga
Rasilimali
watu ni changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya nchini Tanzania.
Upungufu huu unaathiri mfumo wa utoaji huduma bora na kwa wakati kwa
wahitaji. Upungufu wa wahudumu wa afya wenye ujuzi unaathiri ngazi zote
za huduma na hasa vijijini. Kutokana na wauguzi wakunga kuwa kiini
katika utoaji huduma za afya vijijini na mijini kwa ujumla, kuna
umuhimu wa wakunga hawa kupata elimu ya ujuzi wa kutosha ili waweze
kuwafikia wahitaji zaidi ya asilimia sabini (70%) ya jumla ya
wananchi wanaoishi vijijini.
Katika
kupambana na changamoto ya upungufu wa wahudumu wa afya hasa katika
kulenga kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, Amref
Health Africa imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha taasisi,
mashirika na watu binafsi kuchangia mafunzo ya wakunga watalaam ili
waweze kutoa huduma salama, sahihi na kwa wakati ili kupunguza vifo
vinavyoweza kuepukika wakati wa kujifungua.
Jumla
ya Wanafunzi 121 wamehitimu mafunzo ya uuguzi ukunga ngazi ya cheti
katika chuo cha Muheza School of Nursing mkoani Tanga. Miongoni mwa
wanafunzi hao 9 walikuwa wakisoma kwa udhamini wa Barclays bank kupitia
kampeni ya “Stand up for African Mothers” inayoendeshwa na Shirika la
afya la Amref Health Africa Tanzania.
Barclays
Bank ni mshiriki mkubwa katika kampeni hii na anatoa udhamini wa
kusomesha wanafunzi katika ngazi ya cheti na hivi leo tumeshuhudia
wanafunzi 9 wamehitimu tayari kwa kwenda kutoa huduma katika jamii
zinazowazunguka. Wahitimu hawa wanakwenda kufanya kazi maeneo ya
vijijini Kama moja ya lengo na nia ya kampeni ya stand up for African
mothers ambayo inalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto hasa maeneo ya
kijijini na yaliyo magumu kufikika.
Juhudi
za Amref Health Africa na Barclays bank ni endelevu na wito unatolewa
kwa mashirika, makampuni ya umma na yale ya binafsi, pamoja na watu
binafsi kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga
(mafunzo ya mkunga kwa miaka miwili yanagharimu dola 3000). Unaweza
kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia
• Bank account at Bank M, Kisutu Branch , Akaunti Namba 0250027331
• Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548
• Mpesa Namba 0762 22 33 48
• Tigo pesa Namba 0716 032 441
• Airtel money Namba 0685 506306.
Stand
Up For African mothers ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuelimisha na
kutoa taarifa juu ya umuhimu na mchango wa wakunga wenye ujuzi katika
kupunguza viofo vya mama na watoto wakati wa kujifungua. Kampeni hii
inayoendeshwa na Amref Health Africa inalenga kusomesha wakunga 15,000
katika nchi kumi na tatu za Africa wakati Tanzania ikitarajia kusomesha
wakunga 3800.
Dr.
Pius Chaya,mkuu wa kitengo cha kujenga uwezo Amref Health Africa
Tanzania akimuwakilisha Mkurugenzi , Dr. Festus Ilako wakati wa
mahafali Chuo hapo.
Jumla
ya wanafunzi 121 waliohitimu uuguzi ngazi ya Cheti, miongoni mwao
wakiwemo tisa (9) waliofadhiliwa na Barclays kupitia Stand u For
African Mothers Campaign inayoendeshwa na Amref Healt.
Mkuu wa Chuo akiwa pamoja na viongozi, wakufunzi wengine katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Chuo, Baba Askofu pamoja na viongozi wa madhehebu mengine katika picha ya pmaoja.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA WATAALAMU WA UGAVI JIJINI ARUSHA
Mwandishi wetu,Arusha
WIZARA
ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa Ugavi na Manunuzi nchni
(PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia
thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja kuwaajiri
watu wasio na sifa kufanya kazi hizo
Naibu
Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua
mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la
Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia
maadili na miiko ya kazi yao.
Amesema
katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni
20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya
bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee
katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya
mkutano huo “Thamani halisi ya fedha za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha
serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua
uchumi wa nchi.
Amesema
Bodi hiyo imezalisha wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali
ambayo ni sawa na asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri
watumishi wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa Bodi ya Wataalamu wa
Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa Siku mbili unaofanyika kwenye
kituo cha mikutano cha AICC, jijini Arusha.
Naibu
Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa Siku
mbili wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) unaofanyika
kwenye kituo cha mikutano cha AICC jijini Arusha..jpg)
.jpg)
Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence
Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba
nzuri.
Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha
CLOUDS FM YASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWAKE.
Mmoja
wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo
mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na
ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya
kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake
nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na
mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na
pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
Msanii
mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha
ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15
tangu kuanzishwa kwake nchini.
Mkuu
wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya
Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa
kipindi cha XXL,Dj Fetty.
Dj
Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo
ya kutimizwa miaka 15 kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na
kwingineko.
Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa
kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka
15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
Msanii wa zamani wa Bongofleva aliyewahi kuwa kwenye kundi la B Love M,Masiga Msigalla
Kulikuwepo na wimbo wa kuimba pamoja
Ndafu wa shughuli akiwa mezani
Ndafu akitolewa nje ili aliwe vizuri
Wadau mbalimbali pia walikuwepo.
Shayo akihakikisha kila mmoja anapata kipande cha Ndafu
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akihojiwa machache na Mtangazaji wa Clouds TV,Antonia Nugaz
Kutoka Idara ya Muziki Clouds FM,anaitwa Othman Suka na Da Husna mtangazaji wa kipindi Leo Tena
Mrope nae akigawa vipande vya Ndafu
Kutabasamu,kuwhatsapika pia kulikwepo mjengoni hapa
''Heee hii imetoka vizuuuriiii..''
Adam
Mchovu akiwatangazia baadhi ya wafanyakazi wenzake kuhusiana na
utaraibu mzima wa kwenda kujiachia kwenye kiota cha maraha cha Escape
One.
Mazungumzo ya hapa na pale ya kishosti yalinoga pia huku ndafu akiliwa taratibuu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)



















No comments:
Post a Comment